Yeremia 2:3
Jeremiah 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Israeli alikuwa mtakatifu kwa Bwana, kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake; wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia, nayo maafa yaliwakumba,’ ” asema Bwana.
Jeremiah 2:3 in English
Jeremiah 2:3 · Berean Standard Bible
Israel was holy to the LORD, the firstfruits of His harvest. All who devoured her found themselves guilty; disaster came upon them,’” declares the LORD.
Context
1Neno la Bwana lilinijia kusema, 2“Nenda ukahubiri masikioni mwa watu wa Yerusalemu:
“ ‘Nakumbuka moyo wako wa uchaji katika ujana wako,
jinsi ulivyonipenda kama bibi arusi
na kunifuata katika jangwa lile lote,
katika nchi isiyopandwa mbegu. 3Israeli alikuwa mtakatifu kwa Bwana,
kama malimbuko ya kwanza ya mavuno yake;
wote waliowaangamiza walihesabiwa kuwa na hatia,
nayo maafa yaliwakumba,’ ”
asema Bwana. 4Sikia neno la Bwana, ee nyumba ya Yakobo,
nanyi nyote jamaa za nyumba ya Israeli. 5Hivi ndivyo asemavyo Bwana:
“Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu,
hata wakatangatanga mbali nami hivyo?
Walifuata sanamu zisizofaa,
nao wenyewe wakawa hawafai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.