Native Bible

Jeremiah 2:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Sasa kwa nini uende Misri kunywa maji ya Shihori?* Nawe kwa nini kwenda Ashuru kunywa maji ya Mto Frati?

Jeremiah 2:18 in English

Jeremiah 2:18 · Berean Standard Bible

Now what will you gain on your way to Egypt to drink the waters of the Nile *? What will you gain on your way to Assyria to drink the waters of the Euphrates *?

Context

16Pia watu wa Memfisi* na Tahpanhesi* wamevunja taji ya kichwa chako. 17Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe kwa kumwacha Bwana, Mungu wako alipowaongoza njiani? 18Sasa kwa nini uende Misri kunywa maji ya Shihori?* Nawe kwa nini kwenda Ashuru kunywa maji ya Mto Frati? 19Uovu wako utakuadhibu; kurudi nyuma kwako kutakukemea. Basi kumbuka, utambue jinsi lilivyo ovu na chungu kwako unapomwacha Bwana Mungu wako na kutokuwa na hofu yangu,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote. 20“Zamani nilivunja nira yako na kukatilia mbali vifungo vyako; ukasema, ‘Sitakutumikia!’ Naam kweli, kwenye kila kilima kirefu na chini ya kila mti uliotanda matawi yake ulijilaza kama kahaba.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.