Yeremia 2:17
Jeremiah 2:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe kwa kumwacha Bwana, Mungu wako alipowaongoza njiani?
Jeremiah 2:17 in English
Jeremiah 2:17 · Berean Standard Bible
Have you not brought this on yourself by forsaking the LORD your God when He led you in the way?
Context
15Simba wamenguruma;
wamemngurumia.
Wameifanya nchi yake kuwa ukiwa;
miji yake imeteketezwa, nayo imeachwa haina watu. 16Pia watu wa Memfisi* na Tahpanhesi*
wamevunja taji ya kichwa chako. 17Je, hukujiletea hili wewe mwenyewe
kwa kumwacha Bwana, Mungu wako
alipowaongoza njiani? 18Sasa kwa nini uende Misri
kunywa maji ya Shihori?*
Nawe kwa nini kwenda Ashuru
kunywa maji ya Mto Frati? 19Uovu wako utakuadhibu;
kurudi nyuma kwako kutakukemea.
Basi kumbuka, utambue
jinsi lilivyo ovu na chungu kwako
unapomwacha Bwana Mungu wako
na kutokuwa na hofu yangu,”
asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.