Yeremia 10:8
Jeremiah 10:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wote hawana akili, tena ni wapumbavu, wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lolote.
Jeremiah 10:8 in English
Jeremiah 10:8 · Berean Standard Bible
But they are altogether senseless and foolish, instructed by worthless idols made of wood!
Context
6Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana;
wewe ni mkuu,
jina lako ni lenye nguvu katika uweza. 7Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe,
Ee Mfalme wa mataifa?
Hii ni stahili yako.
Miongoni mwa watu wote wenye hekima
katika mataifa na katika falme zao zote,
hakuna aliye kama wewe. 8Wote hawana akili, tena ni wapumbavu,
wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lolote. 9Huleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi
na dhahabu kutoka Ufazi.
Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza
huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani:
vyote vikiwa vimetengenezwa
na mafundi stadi. 10Lakini Bwana ni Mungu wa kweli,
yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele.
Anapokasirika, dunia hutetemeka,
mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.