Yeremia 10:6
Jeremiah 10:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana; wewe ni mkuu, jina lako ni lenye nguvu katika uweza.
Jeremiah 10:6 in English
Jeremiah 10:6 · Berean Standard Bible
There is none like You, O LORD. You are great, and Your name is mighty in power.
Context
4Wanaparemba kwa fedha na dhahabu,
wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike. 5Sanamu zao ni kama sanamu
iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege
nazo haziwezi kuongea;
sharti zibebwe
sababu haziwezi kutembea.
Usiziogope; haziwezi kudhuru,
wala kutenda lolote jema.” 6Hakuna aliye kama wewe, Ee Bwana;
wewe ni mkuu,
jina lako ni lenye nguvu katika uweza. 7Ni nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe,
Ee Mfalme wa mataifa?
Hii ni stahili yako.
Miongoni mwa watu wote wenye hekima
katika mataifa na katika falme zao zote,
hakuna aliye kama wewe. 8Wote hawana akili, tena ni wapumbavu,
wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lolote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.