Yeremia 10:19
Jeremiah 10:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu! Jeraha langu ni kubwa! Lakini nilisema, “Kweli hii ni adhabu yangu, nami sharti niistahimili.”
Jeremiah 10:19 in English
Jeremiah 10:19 · Berean Standard Bible
Woe to me because of my brokenness; my wound is grievous! But I said, “This is truly my sickness, and I must bear it.”
Context
17Kusanyeni mali na vitu vyenu mwondoke nchi hii,
enyi mnaoishi katika hali ya kuzingirwa na jeshi. 18Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:
“Wakati huu, nitawatupa nje kwa nguvu
wote waishio katika nchi hii;
nitawataabisha
ili waweze kutekwa.” 19Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu!
Jeraha langu ni kubwa!
Lakini nilisema,
“Kweli hii ni adhabu yangu,
nami sharti niistahimili.” 20Hema langu limeangamizwa;
kamba zake zote zimekatwa.
Wana wangu wametekwa na hawapo tena;
hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu
wala wa kusimamisha kibanda changu. 21Wachungaji hawana akili
wala hawamuulizi Bwana,
hivyo hawastawi
na kundi lao lote la kondoo limetawanyika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.