Yeremia 10:21
Jeremiah 10:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wachungaji hawana akili wala hawamuulizi Bwana, hivyo hawastawi na kundi lao lote la kondoo limetawanyika.
Jeremiah 10:21 in English
Jeremiah 10:21 · Berean Standard Bible
For the shepherds have become senseless; they do not seek the LORD. Therefore they have not prospered, and all their flock is scattered.
Context
19Ole wangu mimi kwa ajili ya kuumia kwangu!
Jeraha langu ni kubwa!
Lakini nilisema,
“Kweli hii ni adhabu yangu,
nami sharti niistahimili.” 20Hema langu limeangamizwa;
kamba zake zote zimekatwa.
Wana wangu wametekwa na hawapo tena;
hakuna hata mmoja aliyebaki wa kusimamisha hema langu
wala wa kusimamisha kibanda changu. 21Wachungaji hawana akili
wala hawamuulizi Bwana,
hivyo hawastawi
na kundi lao lote la kondoo limetawanyika. 22Sikilizeni! Taarifa inakuja:
ghasia kubwa kutoka nchi ya kaskazini!
Hii itafanya miji ya Yuda ukiwa,
makao ya mbweha. 23Ninajua, Ee Bwana, kwamba maisha ya mwanadamu si yake mwenyewe;
hawezi kuziongoza hatua zake mwenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.