Yeremia 1:7
Jeremiah 1:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Bwana akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza.
Jeremiah 1:7 in English
Jeremiah 1:7 · Berean Standard Bible
But the LORD told me: “Do not say, ‘I am only a child.’ For to everyone I send you, you must go, and all that I command you, you must speak.
Context
5“Kabla sijakuumba ndani ya tumbo la mama yako, nilikujua;
kabla hujazaliwa nilikutenga kwa kazi maalum;
nilikuweka uwe nabii kwa mataifa.” 6Nami nikasema, “Aa, Bwana Mwenyezi, sijui kusema, kwani mimi ni mtoto mdogo tu.” 7Lakini Bwana akaniambia, “Usiseme, ‘Mimi ni mtoto mdogo tu.’ Utaenda popote nitakapokutuma na kunena lolote nitakalokuagiza. 8Usiwaogope, kwa maana niko pamoja nawe nikuokoe,” asema Bwana. 9Kisha Bwana akaunyoosha mkono wake na kugusa kinywa changu, akaniambia, “Sasa nimeyaweka maneno yangu kinywani mwako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.