Native Bible

Isaiah 9:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo, utamwangukia Israeli.

Isaiah 9:8 in English

Isaiah 9:8 · Berean Standard Bible

The Lord has sent a message against Jacob, and it has fallen upon Israel.

Context

6Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanaume, nao utawala utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. 7Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala katika kiti cha enzi cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote utatimiza haya. 8Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo, utamwangukia Israeli. 9Watu wote watajua hili: Efraimu na wakazi wa Samaria, wanaosema kwa kiburi na majivuno ya mioyo, 10“Matofali yameanguka chini, lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa, mitini imeangushwa, lakini tutapanda mierezi badala yake.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.