Native Bible

Isaiah 9:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Matofali yameanguka chini, lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa, mitini imeangushwa, lakini tutapanda mierezi badala yake.”

Isaiah 9:10 in English

Isaiah 9:10 · Berean Standard Bible

“The bricks have fallen, but we will rebuild with finished stone; the sycamores have been felled, but we will replace them with cedars.”

Context

8Bwana ametuma ujumbe dhidi ya Yakobo, utamwangukia Israeli. 9Watu wote watajua hili: Efraimu na wakazi wa Samaria, wanaosema kwa kiburi na majivuno ya mioyo, 10“Matofali yameanguka chini, lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa, mitini imeangushwa, lakini tutapanda mierezi badala yake.” 11Lakini Bwana amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao na kuchochea watesi wao. 12Waashuru kutoka upande wa mashariki na Wafilisti kutoka upande wa magharibi wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa. Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali, mkono wake bado umeinuliwa juu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.