Isaya 9:11
Isaiah 9:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Bwana amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao na kuchochea watesi wao.
Isaiah 9:11 in English
Isaiah 9:11 · Berean Standard Bible
The LORD has raised up the foes of Rezin against him and joined his enemies together.
Context
9Watu wote watajua hili:
Efraimu na wakazi wa Samaria,
wanaosema kwa kiburi
na majivuno ya mioyo, 10“Matofali yameanguka chini,
lakini tutajenga tena kwa mawe yaliyochongwa,
mitini imeangushwa,
lakini tutapanda mierezi badala yake.” 11Lakini Bwana amemtia nguvu adui wa Resini dhidi yao
na kuchochea watesi wao. 12Waashuru kutoka upande wa mashariki
na Wafilisti kutoka upande wa magharibi
wameila Israeli kwa kinywa kilichopanuliwa.
Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu. 13Lakini watu hawajamrudia yeye aliyewapiga,
wala hawajamtafuta Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.