Native Bible

Isaiah 8:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Kwa sababu watu hawa wamekataa maji ya Shilo yatiririkayo taratibu wakamfurahia Resini na mwana wa Remalia,

Isaiah 8:6 in English

Isaiah 8:6 · Berean Standard Bible

“Because this people has rejected the gently flowing waters of Shiloah and rejoiced in Rezin and the son of Remaliah,

Context

4Kabla mtoto hajaweza kusema ‘Baba yangu’ au ‘Mama yangu,’ utajiri wa Dameski na nyara za Samaria zitachukuliwa na mfalme wa Ashuru.” 5Bwana akasema nami tena: 6“Kwa sababu watu hawa wamekataa maji ya Shilo yatiririkayo taratibu wakamfurahia Resini na mwana wa Remalia, 7kwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao mafuriko makubwa ya Mto:* yaani mfalme wa Ashuru na fahari yake yote. Yatafurika juu ya mifereji yake yote, yatamwagikia juu ya kingo zake zote, 8na kufika hadi Yuda, yakizunguka kwa kasi juu yake, yakipita katikati na yakifika hadi shingoni. Mabawa yake yaliyokunjuliwa yatafunika upana wa nchi yako, Ee Imanueli!”*

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.