Native Bible

Isaiah 8:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

kwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao mafuriko makubwa ya Mto:* yaani mfalme wa Ashuru na fahari yake yote. Yatafurika juu ya mifereji yake yote, yatamwagikia juu ya kingo zake zote,

Isaiah 8:7 in English

Isaiah 8:7 · Berean Standard Bible

the Lord will surely bring against them the mighty floodwaters of the Euphrates *— the king of Assyria and all his pomp. It will overflow its channels and overrun its banks.

Context

5Bwana akasema nami tena: 6“Kwa sababu watu hawa wamekataa maji ya Shilo yatiririkayo taratibu wakamfurahia Resini na mwana wa Remalia, 7kwa hiyo Bwana yu karibu kuleta dhidi yao mafuriko makubwa ya Mto:* yaani mfalme wa Ashuru na fahari yake yote. Yatafurika juu ya mifereji yake yote, yatamwagikia juu ya kingo zake zote, 8na kufika hadi Yuda, yakizunguka kwa kasi juu yake, yakipita katikati na yakifika hadi shingoni. Mabawa yake yaliyokunjuliwa yatafunika upana wa nchi yako, Ee Imanueli!”* 9Inueni kilio cha vita, enyi mataifa, na mkavunjwevunjwe! Sikilizeni, enyi nyote nchi za mbali. Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe! Jiandaeni kwa vita, nanyi mkavunjwevunjwe!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.