Isaya 66:11
Isaiah 66:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka katika faraja ya matiti yake; mtakunywa sana, na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.”
Isaiah 66:11 in English
Isaiah 66:11 · Berean Standard Bible
so that you may nurse and be satisfied at her comforting breasts; you may drink deeply and delight yourselves in her glorious abundance.
Context
9Je, nilete mwana hadi wakati wa kuzaliwa
na nisizalishe?” asema Bwana.
“Je, nifunge tumbo la uzazi
wakati mimi ndiye nizalishaye?”
asema Mungu wako. 10“Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake,
ninyi nyote mnaompenda,
shangilieni kwa nguvu pamoja naye,
ninyi nyote mnaoomboleza juu yake. 11Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka
katika faraja ya matiti yake;
mtakunywa sana,
na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.” 12Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:
“Nitamwongezea amani kama mto,
nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho;
utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake
na kubembelezwa magotini pake. 13Kama mama anavyomfariji mtoto wake,
ndivyo nitakavyokufariji wewe,
nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.