Isaya 66:13
Isaiah 66:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama mama anavyomfariji mtoto wake, ndivyo nitakavyokufariji wewe, nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.”
Isaiah 66:13 in English
Isaiah 66:13 · Berean Standard Bible
As a mother comforts her son, so will I comfort you, and you will be consoled over Jerusalem.”
Context
11Kwa kuwa mtanyonya na kutosheka
katika faraja ya matiti yake;
mtakunywa sana,
na kuufurahia wingi wa mafuriko ya ustawi wake.” 12Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:
“Nitamwongezea amani kama mto,
nao utajiri wa mataifa kama kijito kifurikacho;
utanyonya na kuchukuliwa mikononi mwake
na kubembelezwa magotini pake. 13Kama mama anavyomfariji mtoto wake,
ndivyo nitakavyokufariji wewe,
nawe utafarijiwa huko Yerusalemu.” 14Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia,
nanyi mtastawi kama majani;
mkono wa Bwana utajulikana kwa watumishi wake,
bali ghadhabu yake kali
itaonyeshwa kwa adui zake. 15Tazama, Bwana anakuja na moto,
magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli,
atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali,
na karipio lake pamoja na miali ya moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.