Isaya 61:5
Isaiah 61:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wageni watayachunga makundi yenu, wageni watafanya kazi katika mashamba yenu, na kutunza mashamba yenu ya mizabibu.
Isaiah 61:5 in English
Isaiah 61:5 · Berean Standard Bible
Strangers will stand and feed your flocks, and foreigners will be your plowmen and vinedressers.
Context
3na kuwapa mahitaji
wale wanaohuzunika katika Sayuni,
ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu,
mafuta ya furaha badala ya maombolezo,
vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.
Nao wataitwa mialoni ya haki,
pando la Bwana,
ili kuonyesha utukufu wake. 4Watajenga upya magofu ya zamani
na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani;
watafanya upya miji iliyoharibiwa,
iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi. 5Wageni watayachunga makundi yenu,
wageni watafanya kazi katika mashamba yenu,
na kutunza mashamba yenu ya mizabibu. 6Nanyi mtaitwa makuhani wa Bwana,
mtaitwa watumishi wa Mungu wetu.
Mtakula utajiri wa mataifa,
nanyi katika utajiri wao mtajisifu. 7Badala ya aibu yao
watu wangu watapokea sehemu maradufu,
na badala ya fedheha
watafurahia katika urithi wao;
hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao,
nayo furaha ya milele itakuwa yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.