Isaya 61:7
Isaiah 61:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Badala ya aibu yao watu wangu watapokea sehemu maradufu, na badala ya fedheha watafurahia katika urithi wao; hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao, nayo furaha ya milele itakuwa yao.
Isaiah 61:7 in English
Isaiah 61:7 · Berean Standard Bible
Instead of shame, My people will have a double portion, and instead of humiliation, they will rejoice in their share; and so they will inherit a double portion in their land, and everlasting joy will be theirs.
Context
5Wageni watayachunga makundi yenu,
wageni watafanya kazi katika mashamba yenu,
na kutunza mashamba yenu ya mizabibu. 6Nanyi mtaitwa makuhani wa Bwana,
mtaitwa watumishi wa Mungu wetu.
Mtakula utajiri wa mataifa,
nanyi katika utajiri wao mtajisifu. 7Badala ya aibu yao
watu wangu watapokea sehemu maradufu,
na badala ya fedheha
watafurahia katika urithi wao;
hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao,
nayo furaha ya milele itakuwa yao. 8“Kwa maana Mimi, Bwana, napenda haki,
na ninachukia unyangʼanyi na uovu.
Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao
na kufanya agano la milele nao. 9Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa,
na uzao wao miongoni mwa kabila za watu.
Wale wote watakaowaona watatambua
kuwa ni taifa ambalo Bwana amelibariki.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.