Native Bible

Isaiah 60:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Ni nani hawa warukao kama mawingu, kama hua kuelekea kwenye viota vyao?

Isaiah 60:8 in English

Isaiah 60:8 · Berean Standard Bible

Who are these who fly like clouds, like doves to their shelters?

Context

6Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako, ngamia vijana wa Midiani na Efa. Nao wote watokao Sheba watakuja, wakichukua dhahabu na uvumba na kutangaza sifa za Bwana. 7Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia, watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu, nami nitalipamba Hekalu langu tukufu. 8“Ni nani hawa warukao kama mawingu, kama hua kuelekea kwenye viota vyao? 9Hakika visiwa vinanitazama, merikebu za Tarshishi* ndizo zinazotangulia, zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, wakiwa na fedha na dhahabu zao, kwa heshima ya Bwana, Mungu wenu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekujalia utukufu. 10“Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonyesha huruma.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.