Native Bible

Isaiah 60:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonyesha huruma.

Isaiah 60:10 in English

Isaiah 60:10 · Berean Standard Bible

Foreigners will rebuild your walls, and their kings will serve you. Although I struck you in anger, yet in favor I will show you mercy.

Context

8“Ni nani hawa warukao kama mawingu, kama hua kuelekea kwenye viota vyao? 9Hakika visiwa vinanitazama, merikebu za Tarshishi* ndizo zinazotangulia, zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, wakiwa na fedha na dhahabu zao, kwa heshima ya Bwana, Mungu wenu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekujalia utukufu. 10“Wageni watazijenga upya kuta zako, na wafalme wao watakutumikia. Ingawa katika hasira nilikupiga, lakini katika upendeleo wangu nitakuonyesha huruma. 11Malango yako yatakuwa wazi siku zote, kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku, ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa: wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi. 12Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia; utaharibiwa kabisa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.