Isaya 60:12
Isaiah 60:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia; utaharibiwa kabisa.
Isaiah 60:12 in English
Isaiah 60:12 · Berean Standard Bible
For the nation or kingdom that will not serve you will perish; it will be utterly destroyed.
Context
10“Wageni watazijenga upya kuta zako,
na wafalme wao watakutumikia.
Ingawa katika hasira nilikupiga,
lakini katika upendeleo wangu
nitakuonyesha huruma. 11Malango yako yatakuwa wazi siku zote,
kamwe hayatafungwa, mchana wala usiku,
ili watu wapate kukuletea utajiri wa mataifa:
wafalme wao wakiongoza maandamano ya ushindi. 12Kwa maana taifa au ufalme ule ambao hautakutumikia utaangamia;
utaharibiwa kabisa. 13“Utukufu wa Lebanoni utakujilia,
msunobari, mvinje pamoja na mteashuri,
ili kupapamba mahali pangu patakatifu,
nami nitapatukuza mahali pa miguu yangu. 14Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako,
wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako,
nao watakuita Mji wa Bwana,
Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.