Isaya 60:3
Isaiah 60:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako.
Isaiah 60:3 in English
Isaiah 60:3 · Berean Standard Bible
Nations will come to your light, and kings to the brightness of your dawn.
Context
1“Ondoka, angaza, kwa kuwa nuru yako imekuja
na utukufu wa Bwana umezuka juu yako. 2Tazama, giza litaifunika dunia
na giza kuu litayafunika mataifa,
lakini Bwana atazuka juu yako
na utukufu wake utaonekana juu yako. 3Mataifa watakuja kwenye nuru yako
na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako. 4“Inua macho yako na utazame pande zote:
Wote wanakusanyika na kukujia,
wana wako wanakuja toka mbali,
nao binti zako wanabebwa mikononi. 5Ndipo utatazama na kutiwa nuru,
moyo wako utasisimka na kujaa furaha,
mali zilizo baharini zitaletwa kwako,
utajiri wa mataifa utakujilia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.