Native Bible

Isaiah 60:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Inua macho yako na utazame pande zote: Wote wanakusanyika na kukujia, wana wako wanakuja toka mbali, nao binti zako wanabebwa mikononi.

Isaiah 60:4 in English

Isaiah 60:4 · Berean Standard Bible

Lift up your eyes and look around: They all gather and come to you; your sons will come from afar, and your daughters will be carried on the arm.

Context

2Tazama, giza litaifunika dunia na giza kuu litayafunika mataifa, lakini Bwana atazuka juu yako na utukufu wake utaonekana juu yako. 3Mataifa watakuja kwenye nuru yako na wafalme kwa mwanga wa mapambazuko yako. 4“Inua macho yako na utazame pande zote: Wote wanakusanyika na kukujia, wana wako wanakuja toka mbali, nao binti zako wanabebwa mikononi. 5Ndipo utatazama na kutiwa nuru, moyo wako utasisimka na kujaa furaha, mali zilizo baharini zitaletwa kwako, utajiri wa mataifa utakujilia. 6Makundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako, ngamia vijana wa Midiani na Efa. Nao wote watokao Sheba watakuja, wakichukua dhahabu na uvumba na kutangaza sifa za Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.