Isaya 57:3
Isaiah 57:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Lakini ninyi: Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi, ninyi wazao wa wazinzi na makahaba!
Isaiah 57:3 in English
Isaiah 57:3 · Berean Standard Bible
“But come here, you sons of a sorceress, you offspring of adulterers and prostitutes!
Context
1Mwenye haki hupotea,
wala hakuna hata mmoja awazaye hilo moyoni mwake;
watu wanaomcha Mungu huondolewa,
wala hakuna hata mmoja anayeelewa
kuwa wenye haki wameondolewa
ili wasipatikane na maovu. 2Wale waendao kwa unyofu
huwa na amani;
hupata pumziko walalapo mautini. 3“Lakini ninyi:
Njooni hapa, ninyi wana wa wachawi,
ninyi wazao wa wazinzi na makahaba! 4Mnamdhihaki nani?
Ni nani mnayemcheka kwa dharau,
na kumtolea ndimi zenu?
Je, ninyi si watoto wa waasi,
uzao wa waongo? 5Mnawaka tamaa katikati ya mialoni
na chini ya kila mti uliotanda matawi;
mnawatoa kafara watoto wenu kwenye mabonde
na chini ya majabali yenye mianya.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.