Isaya 52:2
Isaiah 52:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Jikungʼute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu. Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako, ee Binti Sayuni uliye mateka.
Isaiah 52:2 in English
Isaiah 52:2 · Berean Standard Bible
Shake off your dust! Rise up and sit on your throne, O Jerusalem. Remove the chains from your neck, O captive Daughter of Zion.
Context
1Amka, amka, ee Sayuni,
jivike nguvu.
Vaa mavazi yako ya fahari,
ee Yerusalemu, mji mtakatifu.
Asiyetahiriwa na aliye najisi
hataingia kwako tena. 2Jikungʼute mavumbi yako,
inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu.
Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako,
ee Binti Sayuni uliye mateka. 3Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana:
“Mliuzwa pasipo malipo,
nanyi mtakombolewa bila fedha.” 4Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:
“Hapo kwanza watu wangu walishuka Misri kuishi,
hatimaye, Ashuru wakawaonea.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.