Native Bible

Isaiah 52:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: “Hapo kwanza watu wangu walishuka Misri kuishi, hatimaye, Ashuru wakawaonea.

Isaiah 52:4 in English

Isaiah 52:4 · Berean Standard Bible

For this is what the Lord GOD says: “At first My people went down to Egypt to live, then Assyria oppressed them without cause.

Context

2Jikungʼute mavumbi yako, inuka, uketi kwenye kiti cha enzi, ee Yerusalemu. Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako, ee Binti Sayuni uliye mateka. 3Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana: “Mliuzwa pasipo malipo, nanyi mtakombolewa bila fedha.” 4Kwa maana hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi: “Hapo kwanza watu wangu walishuka Misri kuishi, hatimaye, Ashuru wakawaonea. 5“Basi sasa nina nini hapa?” asema Bwana. “Kwa kuwa watu wangu wamechukuliwa pasipo malipo, nao wale wanaowatawala wanawadhihaki,” asema Bwana. “Mchana kutwa jina langu limetukanwa bila kikomo. 6Kwa hiyo watu wangu watalijua Jina langu; kwa hiyo katika siku ile watajua kwamba ndimi niliyetangulia kulisema. Naam, ni mimi.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.