Isaya 49:13
Isaiah 49:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pigeni kelele kwa furaha, enyi mbingu; furahi, ee dunia; pazeni sauti kwa kuimba, enyi milima! Kwa maana Bwana anawafariji watu wake, naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa.
Isaiah 49:13 in English
Isaiah 49:13 · Berean Standard Bible
Shout for joy, O heavens; rejoice, O earth; break forth in song, O mountains! For the LORD has comforted His people, and He will have compassion on His afflicted ones.
Context
11Nitaifanya milima yangu yote kuwa barabara,
na njia kuu zangu zitainuliwa. 12Tazama, watakuja kutoka mbali:
wengine kutoka kaskazini, wengine kutoka magharibi,
wengine kutoka nchi ya Sinimu.”* 13Pigeni kelele kwa furaha, enyi mbingu;
furahi, ee dunia;
pazeni sauti kwa kuimba, enyi milima!
Kwa maana Bwana anawafariji watu wake,
naye atakuwa na huruma kwa watu wake walioumizwa. 14Lakini Sayuni alisema, “Bwana ameniacha,
Bwana amenisahau.” 15“Je, mama aweza kumsahau mtoto
aliyeko matitini mwake akinyonya,
wala asiwe na huruma
juu ya mtoto aliyemzaa?
Ingawa anaweza kusahau,
mimi sitakusahau wewe!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.