Isaya 47:3
Isaiah 47:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Uchi wako utafunuliwa na aibu yako itaonekana. Nitalipa kisasi; sitamhurumia hata mmoja.”
Isaiah 47:3 in English
Isaiah 47:3 · Berean Standard Bible
Your nakedness will be uncovered and your shame will be exposed. I will take vengeance; I will spare no one.”
Context
1“Shuka uketi mavumbini,
ee Bikira Binti Babeli;
keti chini pasipo na kiti cha enzi,
ee binti wa Wakaldayo.
Hutaitwa tena mwororo wala wa kupendeza. 2Chukua mawe ya kusagia, usage unga,
vua shela yako.
Pandisha mavazi yako, ondoa viatu vyako,
vuka vijito kwa shida. 3Uchi wako utafunuliwa
na aibu yako itaonekana.
Nitalipa kisasi;
sitamhurumia hata mmoja.” 4Mkombozi wetu: Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake;
ndiye yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 5“Keti kimya, ingia gizani,
Binti wa Wakaldayo,
hutaitwa tena malkia wa falme.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.