Isaya 47:5
Isaiah 47:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Keti kimya, ingia gizani, Binti wa Wakaldayo, hutaitwa tena malkia wa falme.
Isaiah 47:5 in English
Isaiah 47:5 · Berean Standard Bible
“Sit in silence and go into darkness, O Daughter of Chaldea. For you will no longer be called the queen of kingdoms.
Context
3Uchi wako utafunuliwa
na aibu yako itaonekana.
Nitalipa kisasi;
sitamhurumia hata mmoja.” 4Mkombozi wetu: Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake;
ndiye yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 5“Keti kimya, ingia gizani,
Binti wa Wakaldayo,
hutaitwa tena malkia wa falme. 6Niliwakasirikia watu wangu
na kuaibisha urithi wangu;
niliwatia mikononi mwako,
nawe hukuwaonea huruma.
Hata juu ya wazee
uliweka nira nzito sana. 7Ukasema, ‘Nitaendelea
kuwa malkia milele!’
Lakini hukutafakari mambo haya
wala hukuwaza juu ya kile kingeweza kutokea.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.