Isaya 45:15
Isaiah 45:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hakika wewe u Mungu unayejificha, Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli.
Isaiah 45:15 in English
Isaiah 45:15 · Berean Standard Bible
Truly You are a God who hides Himself, O God of Israel, the Savior.
Context
13Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu:
nitazinyoosha njia zake zote.
Yeye atajenga mji wangu upya,
na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni,
lakini si kwa kulipiwa fedha wala kupewa zawadi,
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.” 14Hili ndilo asemalo Bwana:
“Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi,
nao wale Waseba warefu,
watakujia na kuwa wako,
watakujia wakijikokota nyuma yako,
watakujia wamefungwa minyororo.
Watasujudu mbele yako
wakikusihi na kusema,
‘Hakika Mungu yu pamoja nawe,
wala hakuna mwingine;
hakuna Mungu mwingine.’ ” 15Hakika wewe u Mungu unayejificha,
Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli. 16Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika;
wataenda kutahayarika pamoja. 17Lakini Israeli ataokolewa na Bwana
kwa wokovu wa milele;
kamwe hutaaibika wala kutatahayarika,
milele yote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.