Native Bible

Isaiah 45:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hili ndilo asemalo Bwana: “Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi, nao wale Waseba warefu, watakujia na kuwa wako, watakujia wakijikokota nyuma yako, watakujia wamefungwa minyororo. Watasujudu mbele yako wakikusihi na kusema, ‘Hakika Mungu yu pamoja nawe, wala hakuna mwingine; hakuna Mungu mwingine.’ ”

Isaiah 45:14 in English

Isaiah 45:14 · Berean Standard Bible

This is what the LORD says: “The products of Egypt and the merchandise of Cush,* along with the Sabeans, men of stature, will come over to you and will be yours; they will trudge behind you; they will come over in chains and bow down to you. They will confess to you: ‘God is indeed with you, and there is no other; there is no other God.’”

Context

12Mimi ndiye niliyeumba dunia na kumuumba mwanadamu juu yake. Mikono yangu mwenyewe ndiyo iliyozitanda mbingu, nikayapanga majeshi yake yote ya angani. 13Mimi nitamwinua Koreshi katika haki yangu: nitazinyoosha njia zake zote. Yeye atajenga mji wangu upya, na kuwaweka huru watu wangu walio uhamishoni, lakini si kwa kulipiwa fedha wala kupewa zawadi, asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.” 14Hili ndilo asemalo Bwana: “Mazao ya Misri na bidhaa za Kushi, nao wale Waseba warefu, watakujia na kuwa wako, watakujia wakijikokota nyuma yako, watakujia wamefungwa minyororo. Watasujudu mbele yako wakikusihi na kusema, ‘Hakika Mungu yu pamoja nawe, wala hakuna mwingine; hakuna Mungu mwingine.’ ” 15Hakika wewe u Mungu unayejificha, Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli. 16Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika; wataenda kutahayarika pamoja.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.