Isaya 45:17
Isaiah 45:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini Israeli ataokolewa na Bwana kwa wokovu wa milele; kamwe hutaaibika wala kutatahayarika, milele yote.
Isaiah 45:17 in English
Isaiah 45:17 · Berean Standard Bible
But Israel will be saved by the LORD with an everlasting salvation; you will not be put to shame or humiliated, to ages everlasting.
Context
15Hakika wewe u Mungu unayejificha,
Ee Mungu na Mwokozi wa Israeli. 16Wote watengenezao sanamu wataaibika na kutahayarika;
wataenda kutahayarika pamoja. 17Lakini Israeli ataokolewa na Bwana
kwa wokovu wa milele;
kamwe hutaaibika wala kutatahayarika,
milele yote. 18Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana,
yeye aliyeumba mbingu,
ndiye Mungu;
yeye aliyeifanya dunia na kuiumba,
yeye ndiye aliiwekea misingi imara,
hakuiumba ili iwe tupu,
bali aliiumba ikaliwe na viumbe vyake.
Anasema:
“Mimi ndimi Bwana,
wala hakuna mwingine. 19Sijasema sirini,
kutoka mahali fulani katika nchi ya giza;
sijawaambia wazao wa Yakobo,
‘Nitafuteni bure.’
Mimi, Bwana, nasema kweli;
ninatangaza lililo sahihi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.