Isaya 43:22
Isaiah 43:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Hata hivyo hukuniita mimi, ee Yakobo, hujajitaabisha kwa ajili yangu, ee Israeli.
Isaiah 43:22 in English
Isaiah 43:22 · Berean Standard Bible
But you have not called on Me, O Jacob, because you have grown weary of Me, O Israel.
Context
20Wanyama wa mwituni wataniheshimu,
mbweha na bundi,
kwa sababu ninawapatia maji jangwani,
na vijito katika nchi kame,
ili kuwapa watu wangu maji, wale niliowachagua, 21watu wale niliowaumba kwa ajili yangu,
ili wapate kutangaza sifa zangu. 22“Hata hivyo hukuniita mimi, ee Yakobo,
hujajitaabisha kwa ajili yangu, ee Israeli. 23Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa,
wala kuniheshimu kwa dhabihu zako.
Sikukulemea kwa sadaka za nafaka
wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba. 24Hukuninunulia uvumba wowote wenye manukato,
wala hukunipa kwa ukarimu
mafuta ya wanyama wa dhabihu zako.
Lakini umenilemea kwa dhambi zako,
na kunitaabisha kwa makosa yako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.