Isaya 43:12
Isaiah 43:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nimedhihirisha, kuokoa na kutangaza: Mimi, wala si mungu mgeni katikati yenu. Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana, “kwamba Mimi ndimi Mungu.
Isaiah 43:12 in English
Isaiah 43:12 · Berean Standard Bible
I alone decreed and saved and proclaimed— I, and not some foreign god among you. So you are My witnesses,” declares the LORD, “that I am God.
Context
10“Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana,
“na mtumishi wangu niliyemchagua,
ili mpate kunijua na kuniamini,
na kutambua kwamba Mimi ndiye.
Kabla yangu hakuna mungu aliyefanyizwa,
wala hatakuwepo mwingine baada yangu. 11Mimi, naam mimi, ndimi Bwana,
zaidi yangu hakuna mwokozi. 12Nimedhihirisha, kuokoa na kutangaza:
Mimi, wala si mungu mgeni katikati yenu.
Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana,
“kwamba Mimi ndimi Mungu. 13Naam, tangu siku za kale, Mimi ndiye.
Hakuna hata mmoja awezaye kuokoa
kutoka mkononi wangu.
Mimi ninapotenda,
ni nani awezaye kutangua?” 14Hili ndilo Bwana asemalo,
Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:
“Kwa ajili yenu nitatumana Babeli
na kuwaleta Wakaldayo wote kama wakimbizi,
katika meli walizozionea fahari.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.