Isaya 43:14
Isaiah 43:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo Bwana asemalo, Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli: “Kwa ajili yenu nitatumana Babeli na kuwaleta Wakaldayo wote kama wakimbizi, katika meli walizozionea fahari.
Isaiah 43:14 in English
Isaiah 43:14 · Berean Standard Bible
Thus says the LORD your Redeemer, the Holy One of Israel: “For your sake, I will send to Babylon and bring them all as fugitives, even the Chaldeans,* in the ships in which they rejoice.
Context
12Nimedhihirisha, kuokoa na kutangaza:
Mimi, wala si mungu mgeni katikati yenu.
Ninyi ni mashahidi wangu,” asema Bwana,
“kwamba Mimi ndimi Mungu. 13Naam, tangu siku za kale, Mimi ndiye.
Hakuna hata mmoja awezaye kuokoa
kutoka mkononi wangu.
Mimi ninapotenda,
ni nani awezaye kutangua?” 14Hili ndilo Bwana asemalo,
Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:
“Kwa ajili yenu nitatumana Babeli
na kuwaleta Wakaldayo wote kama wakimbizi,
katika meli walizozionea fahari. 15Mimi ndimi Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wako,
Muumba wa Israeli, Mfalme wako.” 16Hili ndilo asemalo Bwana,
yeye aliyefanya njia baharini,
mahali pa kupita kwenye maji mengi,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.