Isaya 41:23
Isaiah 41:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
tuambieni ni nini kitakachotokea baadaye, ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu. Fanyeni jambo lolote zuri au baya, ili tupate kutishika na kujazwa na hofu.
Isaiah 41:23 in English
Isaiah 41:23 · Berean Standard Bible
Tell us the things that are to come, so that we may know that you are gods. Yes, do something good or evil, that we may look on together in dismay.
Context
21Bwana asema, “Leta shauri lako.
Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo. 22“Leteni sanamu zenu zituambie
ni nini kitakachotokea.
Tuambieni mambo ya zamani yalikuwa nini,
ili tupate kuyatafakari
na kujua matokeo yake ya mwisho.
Au tutangazieni mambo yatakayokuja, 23tuambieni ni nini kitakachotokea baadaye,
ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu.
Fanyeni jambo lolote zuri au baya,
ili tupate kutishika na kujazwa na hofu. 24Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa,
na kazi zenu hazifai kitu kabisa;
yeye awachaguaye ni chukizo sana. 25“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini,
naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu.
Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope,
kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.