Native Bible

Isaiah 41:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana asema, “Leta shauri lako. Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo.

Isaiah 41:21 in English

Isaiah 41:21 · Berean Standard Bible

“Present your case,” says the LORD. “Submit your arguments,” says the King of Jacob.

Context

19Katika jangwa nitaotesha mwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni. Nitaweka misunobari, mivinje na misanduku pamoja huko nyikani, 20ili kwamba watu wapate kuona na kujua, wapate kufikiri na kuelewa, kwamba mkono wa Bwana umetenda hili, kwamba yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ndiye alilifanya.” 21Bwana asema, “Leta shauri lako. Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo. 22“Leteni sanamu zenu zituambie ni nini kitakachotokea. Tuambieni mambo ya zamani yalikuwa nini, ili tupate kuyatafakari na kujua matokeo yake ya mwisho. Au tutangazieni mambo yatakayokuja, 23tuambieni ni nini kitakachotokea baadaye, ili tupate kujua kuwa ninyi ni miungu. Fanyeni jambo lolote zuri au baya, ili tupate kutishika na kujazwa na hofu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.