Isaya 41:19
Isaiah 41:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika jangwa nitaotesha mwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni. Nitaweka misunobari, mivinje na misanduku pamoja huko nyikani,
Isaiah 41:19 in English
Isaiah 41:19 · Berean Standard Bible
I will plant cedars in the wilderness, acacias, myrtles, and olive trees. I will set cypresses * in the desert, elms and boxwood together,
Context
17“Maskini na wahitaji wanatafuta maji,
lakini hayapo,
ndimi zao zimekauka kwa kiu.
Lakini Mimi Bwana nitawajibu,
Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha. 18Nitaifanya mito itiririke juu ya vilima vilivyo kame,
nazo chemchemi ndani ya mabonde.
Nitaligeuza jangwa liwe mabwawa ya maji,
nayo ardhi iliyokauka kuwa chemchemi za maji. 19Katika jangwa nitaotesha
mwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni.
Nitaweka misunobari, mivinje na misanduku
pamoja huko nyikani, 20ili kwamba watu wapate kuona na kujua,
wapate kufikiri na kuelewa,
kwamba mkono wa Bwana umetenda hili,
kwamba yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ndiye alilifanya.” 21Bwana asema, “Leta shauri lako.
Toa hoja yako,” asema Mfalme wa Yakobo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.