Isaya 41:17
Isaiah 41:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Maskini na wahitaji wanatafuta maji, lakini hayapo, ndimi zao zimekauka kwa kiu. Lakini Mimi Bwana nitawajibu, Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.
Isaiah 41:17 in English
Isaiah 41:17 · Berean Standard Bible
The poor and needy seek water, but there is none; their tongues are parched with thirst. I, the LORD, will answer them; I, the God of Israel, will not forsake them.
Context
15“Tazama, nitakufanya chombo cha kupuria,
kipya na chenye makali, chenye meno mengi.
Utaipura milima na kuiponda
na kuvifanya vilima kuwa kama makapi. 16Utaipepeta, nao upepo utaichukua,
dhoruba itaipeperushia mbali.
Bali wewe utajifurahisha katika Bwana
na katika utukufu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 17“Maskini na wahitaji wanatafuta maji,
lakini hayapo,
ndimi zao zimekauka kwa kiu.
Lakini Mimi Bwana nitawajibu,
Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha. 18Nitaifanya mito itiririke juu ya vilima vilivyo kame,
nazo chemchemi ndani ya mabonde.
Nitaligeuza jangwa liwe mabwawa ya maji,
nayo ardhi iliyokauka kuwa chemchemi za maji. 19Katika jangwa nitaotesha
mwerezi, mshita, mhadasi na mzeituni.
Nitaweka misunobari, mivinje na misanduku
pamoja huko nyikani,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.