Isaya 40:27
Isaiah 40:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa nini unasema, ee Yakobo, nanyi ee Israeli, kulalamika, “Njia yangu imefichwa Bwana asiione, Mungu wangu hajali shauri langu?”
Isaiah 40:27 in English
Isaiah 40:27 · Berean Standard Bible
Why do you say, O Jacob, and why do you assert, O Israel, “My way is hidden from the LORD, and my claim is ignored by my God”?
Context
25“Utanilinganisha mimi na nani?
Au ni nani anayelingana nami?” asema yeye Aliye Mtakatifu. 26Inueni macho yenu mtazame mbinguni:
Ni nani aliyeumba hivi vyote?
Ni yeye aletaye nje jeshi la nyota moja baada ya nyingine
na kuziita kila moja kwa jina lake.
Kwa sababu ya uweza wake mkuu na nguvu zake kuu,
hakuna hata mojawapo inayokosekana. 27Kwa nini unasema, ee Yakobo,
nanyi ee Israeli, kulalamika,
“Njia yangu imefichwa Bwana asiione,
Mungu wangu hajali shauri langu?” 28Je wewe, hufahamu?
Je wewe, hujasikia?
Bwana ni Mungu wa milele,
Muumba wa miisho ya dunia.
Hatachoka wala kulegea,
wala hakuna hata mmoja
awezaye kuupima ufahamu wake. 29Huwapa nguvu waliolegea
na huongeza nguvu za wadhaifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.