Isaya 40:11
Isaiah 40:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo: Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake na kuwachukua karibu na moyo wake, huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao.
Isaiah 40:11 in English
Isaiah 40:11 · Berean Standard Bible
He tends His flock like a shepherd; He gathers the lambs in His arms and carries them close to His heart. He gently leads the nursing ewes.
Context
9Wewe uletaye habari njema Sayuni,
panda juu ya mlima mrefu.
Wewe uletaye habari njema Yerusalemu,
inua sauti yako kwa kupiga kelele,
inua sauti, usiogope;
iambie miji ya Yuda,
“Yuko hapa Mungu wenu!” 10Tazameni, Bwana Mwenyezi anakuja na nguvu,
nao mkono wake ndio utawalao kwa ajili yake.
Tazameni, ujira wake u pamoja naye,
nayo malipo yake yanafuatana naye. 11Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo:
Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake
na kuwachukua karibu na moyo wake,
huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao. 12Ni nani aliyepima maji ya bahari
kwenye konzi ya mkono wake,
au kuzipima mbingu kwa shibiri* yake?
Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu,
au kupima milima kwenye kipimio
na vilima kwenye mizani? 13Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana,
au kumfundisha akiwa kama mshauri wake?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.