Isaya 40:13
Isaiah 40:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana, au kumfundisha akiwa kama mshauri wake?
Isaiah 40:13 in English
Isaiah 40:13 · Berean Standard Bible
Who has directed the Spirit of the LORD,* or informed Him as His counselor?*
Context
11Huchunga kundi lake kama mchungaji wa mifugo:
Hukusanya wana-kondoo katika mikono yake
na kuwachukua karibu na moyo wake,
huwaongoza taratibu wale wanyonyeshao. 12Ni nani aliyepima maji ya bahari
kwenye konzi ya mkono wake,
au kuzipima mbingu kwa shibiri* yake?
Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu,
au kupima milima kwenye kipimio
na vilima kwenye mizani? 13Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya Bwana,
au kumfundisha akiwa kama mshauri wake? 14Ni nani ambaye Bwana ametaka shauri kwake ili kumwelimisha,
naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa?
Ni nani aliyemfundisha maarifa
au kumwonyesha mapito ya ufahamu? 15Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo,
ni kama vumbi jembamba juu ya mizani,
huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.