Isaya 31:6
Isaiah 31:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana.
Isaiah 31:6 in English
Isaiah 31:6 · Berean Standard Bible
Return to the One against whom you have so blatantly rebelled, O children of Israel.
Context
4Hili ndilo Bwana analoniambia:
“Kama vile simba angurumavyo,
simba mkubwa juu ya mawindo yake:
hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo
huitwa pamoja dhidi yake,
hatiwi hofu na kelele zao
wala kusumbuliwa na ghasia zao;
ndivyo Bwana Mwenye Nguvu Zote atakavyoshuka
kufanya vita juu ya Mlima Sayuni
na juu ya vilele vyake. 5Kama ndege warukao,
Bwana Mwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu;
ataukinga na kuuokoa,
atapita juu yake na kuufanya salama.” 6Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana. 7Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi. 8“Ashuru itaanguka kwa upanga ambao si wa mwanadamu;
upanga usio wa kibinadamu utawaangamiza.
Watakimbia mbele ya upanga
na vijana wao wa kiume watafanyizwa kazi kwa lazima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.