Isaya 31:5
Isaiah 31:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kama ndege warukao, Bwana Mwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu; ataukinga na kuuokoa, atapita juu yake na kuufanya salama.”
Isaiah 31:5 in English
Isaiah 31:5 · Berean Standard Bible
Like birds hovering overhead, so the LORD of Hosts will protect Jerusalem. He will shield it and deliver it; He will pass over it and preserve it.”
Context
3Lakini Wamisri ni wanadamu, wala si Mungu,
farasi wao ni nyama, wala si roho.
Wakati Bwana atakaponyoosha Mkono wake,
yeye anayesaidia atajikwaa,
naye anayesaidiwa ataanguka,
wote wawili wataangamia pamoja. 4Hili ndilo Bwana analoniambia:
“Kama vile simba angurumavyo,
simba mkubwa juu ya mawindo yake:
hata ingawa kundi lote la wachunga mifugo
huitwa pamoja dhidi yake,
hatiwi hofu na kelele zao
wala kusumbuliwa na ghasia zao;
ndivyo Bwana Mwenye Nguvu Zote atakavyoshuka
kufanya vita juu ya Mlima Sayuni
na juu ya vilele vyake. 5Kama ndege warukao,
Bwana Mwenye Nguvu Zote ataukinga Yerusalemu;
ataukinga na kuuokoa,
atapita juu yake na kuufanya salama.” 6Mrudieni yeye ambaye nyumba ya Israeli imemwasi sana. 7Kwa kuwa katika siku ile kila mmoja wenu atazikataa sanamu za fedha na za dhahabu zilizotengenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.