Native Bible

Isaiah 30:31 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Sauti ya Bwana itaivunjavunja Ashuru, kwa fimbo yake ya utawala atawapiga.

Isaiah 30:31 in English

Isaiah 30:31 · Berean Standard Bible

For Assyria will be shattered at the voice of the LORD; He will strike them with His scepter.

Context

29Nanyi mtaimba kama usiku ule mnaadhimisha sikukuu takatifu. Mioyo yenu itashangilia kama vile watu wanapokwea na filimbi kwenye mlima wa Bwana, kwa Mwamba wa Israeli. 30Bwana atawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu, naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka pamoja na hasira yake kali na moto ulao, kukiwa na tufani ya mvua, ngurumo za radi na mvua ya mawe. 31Sauti ya Bwana itaivunjavunja Ashuru, kwa fimbo yake ya utawala atawapiga. 32Kila pigo Bwana atakaloliweka juu yao kwa fimbo yake ya kuadhibu, litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi, anapopigana nao katika vita kwa mapigo ya mkono wake. 33Tofethi imeandaliwa toka zamani, imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme. Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu na kwa upana mkubwa, likiwa na moto na kuni tele; pumzi ya Bwana, kama kijito cha kiberiti, huuwasha moto.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.