Isaya 30:29
Isaiah 30:29 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nanyi mtaimba kama usiku ule mnaadhimisha sikukuu takatifu. Mioyo yenu itashangilia kama vile watu wanapokwea na filimbi kwenye mlima wa Bwana, kwa Mwamba wa Israeli.
Isaiah 30:29 in English
Isaiah 30:29 · Berean Standard Bible
You will sing as on the night of a holy festival, and your heart will rejoice like one who walks to the music of a flute, going up to the mountain of the LORD, to the Rock of Israel.
Context
27Tazama, Jina la Bwana linakuja kutoka mbali,
likiwa na hasira kali inayowaka
pamoja na wingu zito la moshi,
midomo yake imejaa ghadhabu
na ulimi wake ni moto ulao. 28Pumzi yake ni kama mkondo wa maji yaendayo kasi,
yakipanda hadi shingoni.
Hutikisa mataifa katika chekecheke ya uharibifu,
huweka lijamu katika mataya ya mataifa
ambayo huwaongoza upotevuni. 29Nanyi mtaimba kama usiku ule mnaadhimisha
sikukuu takatifu.
Mioyo yenu itashangilia
kama vile watu wanapokwea na filimbi
kwenye mlima wa Bwana,
kwa Mwamba wa Israeli. 30Bwana atawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu,
naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka
pamoja na hasira yake kali na moto ulao,
kukiwa na tufani ya mvua,
ngurumo za radi na mvua ya mawe. 31Sauti ya Bwana itaivunjavunja Ashuru,
kwa fimbo yake ya utawala atawapiga.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.