Isaya 30:32
Isaiah 30:32 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kila pigo Bwana atakaloliweka juu yao kwa fimbo yake ya kuadhibu, litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi, anapopigana nao katika vita kwa mapigo ya mkono wake.
Isaiah 30:32 in English
Isaiah 30:32 · Berean Standard Bible
And with every stroke of the rod of punishment * that the LORD brings down on them, the tambourines and lyres will sound as He battles with weapons brandished.
Context
30Bwana atawasababisha watu waisikie sauti yake ya utukufu,
naye atawafanya wauone mkono wake ukishuka
pamoja na hasira yake kali na moto ulao,
kukiwa na tufani ya mvua,
ngurumo za radi na mvua ya mawe. 31Sauti ya Bwana itaivunjavunja Ashuru,
kwa fimbo yake ya utawala atawapiga. 32Kila pigo Bwana atakaloliweka juu yao
kwa fimbo yake ya kuadhibu,
litakuwa kwa wimbo wa matari na vinubi,
anapopigana nao katika vita
kwa mapigo ya mkono wake. 33Tofethi imeandaliwa toka zamani,
imewekwa tayari kwa ajili ya mfalme.
Shimo lake la moto limetengenezwa kwa kina kirefu
na kwa upana mkubwa,
likiwa na moto na kuni tele;
pumzi ya Bwana,
kama kijito cha kiberiti,
huuwasha moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.