Isaya 30:11
Isaiah 30:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Acheni njia hii, ondokeni katika mapito haya, nanyi acheni kutukabili pamoja na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!”
Isaiah 30:11 in English
Isaiah 30:11 · Berean Standard Bible
Get out of the way; turn off the road. Rid us of the Holy One of Israel!”
Context
9Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu,
watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya Bwana. 10Wanawaambia waonaji,
“Msione maono tena!”
Nako kwa manabii wanasema,
“Msiendelee kutupatia maono
ambayo ni ya kweli!
Tuambieni mambo ya kupendeza,
tabirini mambo ya uongo. 11Acheni njia hii,
ondokeni katika mapito haya,
nanyi acheni kutukabili pamoja
na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!” 12Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:
“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,
mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu, 13dhambi hii itakuwa kwenu
kama ukuta mrefu,
wenye ufa na wenye kubetuka,
ambao unaanguka ghafula,
mara moja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.