Isaya 30:9
Isaiah 30:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu, watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya Bwana.
Isaiah 30:9 in English
Isaiah 30:9 · Berean Standard Bible
These are rebellious people, deceitful children, children unwilling to obey the LORD’s instruction.
Context
7kuvipeleka Misri,
ambaye msaada wake haufai kabisa.
Kwa hiyo nimemwita “Rahabu Asiyefanya Chochote.” 8Nenda sasa, liandike neno hili juu ya kibao kwa ajili yao,
liandike kwenye kitabu,
ili liweze kuwa shahidi milele
kwa ajili ya siku zijazo. 9Hawa ni watu waasi, watoto wadanganyifu,
watoto ambao hawataki kusikiliza mafundisho ya Bwana. 10Wanawaambia waonaji,
“Msione maono tena!”
Nako kwa manabii wanasema,
“Msiendelee kutupatia maono
ambayo ni ya kweli!
Tuambieni mambo ya kupendeza,
tabirini mambo ya uongo. 11Acheni njia hii,
ondokeni katika mapito haya,
nanyi acheni kutukabili pamoja
na yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.