Native Bible

Isaiah 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katika siku ile Bwana atawanyangʼanya uzuri wao: bangili, tepe za kichwani, mikufu yenye alama za mwezi mwandamo,

Isaiah 3:18 in English

Isaiah 3:18 · Berean Standard Bible

In that day the Lord will take away their finery: their anklets and headbands and crescents;

Context

16Bwana asema, “Wanawake wa Sayuni wana kiburi, wanatembea na shingo ndefu, wakikonyeza kwa macho yao, wanatembea kwa hatua za madaha, wakiwa na mapambo ya njuga kwenye vifundo vya miguu yao. 17Kwa hiyo Bwana ataleta majipu kwenye vichwa vya wanawake wa Sayuni; Bwana atazifanya ngozi za vichwa vyao kuwa vipara.” 18Katika siku ile Bwana atawanyangʼanya uzuri wao: bangili, tepe za kichwani, mikufu yenye alama za mwezi mwandamo, 19vipuli, vikuku, shela, 20vilemba, mikufu ya vifundo vya miguu, mshipi, chupa za manukato na hirizi,

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.