Isaya 27:6
Isaiah 27:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku zijazo, Yakobo atatia mizizi, Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua, naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda.
Isaiah 27:6 in English
Isaiah 27:6 · Berean Standard Bible
In the days to come, Jacob will take root. Israel will bud and blossom and fill the whole world with fruit.
Context
4Mimi sijakasirika.
Licha pangekuwepo michongoma na miiba kunikabili!
Ningepambana dhidi yake katika vita,
ningeliichoma moto yote. 5Au niwaache waje kwangu kwa ajili ya kupata kimbilio,
wao na wafanye amani nami,
naam, wafanye amani nami.” 6Katika siku zijazo, Yakobo atatia mizizi,
Israeli atatoa chipukizi na kuchanua maua,
naye atajaza ulimwengu wote kwa matunda. 7Je, Bwana amempiga
vile alivyowapiga wale waliompiga?
Je, yeye ameuawa
vile walivyouawa wale waliomuua yeye? 8Kwa vita na kwa kumfukuza unapingana naye:
kwa mshindo wake mkali anamfukuza,
kama siku ile uvumapo upepo wa mashariki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.